Friday, March 06, 2009

PIGO LA MWISHO DOWANS

Wakati Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Dk Harrison Mwakyembe amesema 'Bora nchi ikae gizani' kuliko kununua mitambo ya Dowans, Mkurugenzi Mtendaji wa Tanesco, Dk Idrisa Rashid 'amenawa' akisema 'Nchi ikiwa gizani, hospitali zikakosa umeme asilaumiwe. Dk Rashid akaongeza: “Mitambo ya umeme hainunuliwi dukani kama gari au trekta ama mavazi hivyo huwezi kwenda kwa watengenezaji ukawambia unataka mtambo na kuupata wakati huo huo au ndani ya wiki mbili kama baadhi ya watu wakiwemo watu wazito wenye majukumu na dhamana kubwa wanavyosema."

No comments:

Post a Comment