Wednesday, March 04, 2009

Mshtakiwa Muhimu Mahututi

HALI ya afya ya Koplo Rashid Lema, mshitakiwa wa 11 katika kesi ya mauaji ya wafanyabiashara watatu na dereva wa teksi, jijini Dar es Salaam, inazidi kuwa mbaya na sasa amelazwa Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH).
Koplo huyo ni shahidi muhimu wa utetezi kulingana na maelezo yake ya awali katika kesi hiyo, kuonyesha fununu za mauaji hayo kuwa yalifanyika katika msitu wa Pande, kwamba yeye alipeleka maiti Muhimbili na inasemekana aliwataja watuhumiwa waliofyatua risasi na jinsi amri ilivyotolewa. Ugonjwa uliotajwa kumkabili mtuhumiwa huyo ni kifua kikuu.
Mwananchi wanayo habari hii na Nipashe wameiandika hivi.

No comments:

Post a Comment