Monday, March 02, 2009

Haki ya Kukanusha

Yule Mkuu wa wilaya ya Maswa, Kapteni mstaafu, James Yamungu, aliyekaririwa akimuunga mkono mwenzake aliyewacharaza walimu bakora kule Bukoba, Albert Mnali soma Mwananchi. Pia akadaiwa kujisifu kwa hatua hiyo soma Tanzania Daima, na kwenye gazeti jingine la tatu jana aliibuka na kukanusha habari hizo kuwa hajawahi kuzitoa mahali popote na kuahidi kuchukua hatua kupitia Baraza la Habari Tanzania (MCT). Gazeti la serikali Habari Leo limempa haki yake ya msingi kukanusha.

No comments:

Post a Comment