Friday, June 16, 2006

Salamu Kutoka 'Makao Makuu'

Nakusalimieni sana wasomaji wangu kutoka 'Makao Makuu' ya nchi Dodoma. Hili ndilo jengo jipya la Bunge, zuri, la thamani kubwa ya sh30.9 bilioni. Ndilo linalovutia sana mjini hapa.(Picha na Mzee wa Sumo)

16 comments:

zemarcopolo said...

hilo jengo linavutia.inagwa tukianzasha mjadala wa kama kweli kuliku na haja wa kulijenga kipindi hiki tena kwa pesa ya mkopo tunaweza tusimalize mwaka huu.je jengo la zamani linatumika kwa shughuli gani hivi sasa?

zemarcopolo said...

ee bwana halafu nilisahau kitu.hiyo jacket yako kaka imekaa mahali pake!!!

John Mwaipopo said...

Litakufaa zaidi pale utakapoingia kama mchangia hoja na sio ripota pale 2010. Tumewachoka vilaza waliorundikana humo kwa pesa na kujuana.

Anonymous said...

Vipi mzee jengo hilo linaendana na hadhi ya Dom? ama limepandikizwa tu hapao.Maana unasema ndilo linalovutia maana yake lina hadhi kubwa kuliko majengo ya Dom sasa vipi ni manazi kati ya michongoma?tse hee hhee aah!Tanzania!

Anonymous said...

Sasa tunaomba akili na mawazo ya wabunge ziendane na jengo hilo, vininevyo mambo mbofumbofu tu.

Boniphace Makene said...

Safi sana Miruko yaani umependeza ungekuwa na microphone na kisha kurusha kitu kama video kama anavyofanya Ndesanjo maana umetoka chicha sana. Pia nashukuru kwa mail ila Komredi Mark Msaki hapatikani hadi sasa.

Reginald S. Miruko said...

Ufafanuzi: Jengo hili limejengwa kwa ushirikiano kati ya Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF) (35%), Mfuko wa Pensheni wa Watumishi wa Umma (PSPF) (30%), Mfuko wa Pensheni wa Mashirika ya Umma (PPF) 25% na Mfuko wa Akiba ya Wafanyakazi wa Serikali za Mitaa (LAPF) wenye asilimia 10.
1. Fedha hizo zitarejeshwa kwa njia ya serikali kupangisha, na wakishapata faida kadri ya makubalino, watalikabidhi moja kwa moja kwa serikali.
2. Majengo la zamani, lilikuwa limejengwa na LAPT kwa gharama ya sh4 bilioni na baada ya miaka kadhaa waliliuza kwa serikali kwa sh9 bilioni. Hivi sasa ukumbi unatumika kwa semina na mikutano mbalimbali. majengo mengine yanaendelea kuwa ofisi za bunge.

mloyi said...

duh! Billioni 31 zimeishia hapo,tunatarajia kwamba litawati uchungu wabungw ili waweze kujadili kwa mapana na marefu hoja zitakazokuwa zinatolewa na vilevile kuibua hoja zilizofichwa kwa lengo la kumnyima mwananchi haki yake.
Cha kusikitisha ni pale tunapoambiwa kwamba jengo lenyewe ni 'bomu' vipaza sauti vimeanza kukataa kufanya kazi(labda vimeshtuka vitatumiwa kuendeleza unyonywaji wa Tanzania) na hiki na kile. Sijui aliyesimamia ujenzi wake atatuambia nini.

Jaduong Metty said...

Jengo zuri, lakini kuna jipya zaidi ya maswali ya kipuuzi toka kwa wabunge?

ndesanjo said...

Salamu tumezipokea!
Mbona bilioni nyingi sana hizo?

Jeff Msangi said...

Wabunge ndio wawakilishi wetu,demokrasia chafu zinasema hivyo.Kama hawakuliona hili la thamani isiyostahili basi hawawezi kuwa wenye msaada wowote kwa majimbo yao ya uchaguzi.Matumizi holela huanzia kwenye mambo kama haya.

charahani said...

Hongera mzee taarifa zako tunazo karibu sana bongo kwanini hauwaagi hao kina Mtangoo, sababu wewe sasa hili koti litakuwa na maana utakapokuwa ndani ya ofisi yako mpya, Huraaa, hivi ulijua nini ndo ukaandika hiki kipisi cha meseji katika dirisha lenye picha yako hapa kulia.

Absalom Kibanda said...

Aise Dodoma ni Makao Makuu ya Bunge na ya CCM si ya nchi Miruko. Hivi sasa Serikali inajenga jengo la mabilioni la Wizara ya Utumishi Dar es Salaam. Jumuiya ya Ulaya imekamilisha jengo la ofisi za nchi wananchi hivi karibuni jijini Dar es Salaam, BoT wanakamilisha Twin Tower lenye thamani ya zaidi ya sh bilioni 150 huko huko Dar es Salaam na kuna mifano mingi kiasi.

Kidogo uamuzi wa KIkwete wa kujenga Chuo Kikuu hapo Dodoma utasaidia kuongeza kasi ya kuboresha mji huo. Hata hivyo huo ni mradi maalum wa kuwapa watu kipato nje ya pato lao

Anonymous said...

Who can help me with .httpaccess ?
where i can fined full information about .httpaccess file syntaxis?

Anonymous said...

MESSAGE

Anonymous said...

hewlett packard digital camera


digital camera samsung digimaxcasio slim digital camera


digital camera samsung digimax

Post a Comment