Sunday, February 22, 2009

Mitambo Dowans yawagawa wabunge



MVUTANO mkali uliibuka jana katika kikao cha Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma na maafisa wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) kuhusiana ombi la kununua mitambo ya kuzalisha umeme inayomilikiwa na Kampuni ya Dowans.





Baadhi ya wabunge wa kamati hiyo iliyokuwa chini ya Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe waliwabana maafisa wa Tanesco waliokuwa wakiongozwa na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika hilo, Dk Idrisa Rashid ili waeleze sababu iliyowafanya waamue kununua mitambo chakavu ya Dowans badala ya mipya.





Wabunge hao walionyesha wasiwasi wao kufuatia nia ya Tanesco kutaka kununua mitambo hiyo huku wakijua kuwa sheria ya manunuzi inazuia ununuzi wa mitambo chakavu.





Soma zaidi hapa







1 comment:

Los Poetas Muertos said...

visit my blog

http://los-poetasmuertos.blogspot.com/

Post a Comment