Tuesday, February 24, 2009

KUMBE YU HAI


Yule mwanamke wa Kihindi, mtuhumiwa wa mauaji aliyedaiwa kufa akiwa gerezani, yu hai na asubuhi hii ametokea kortini Kisutu katika kesi yake. Kuonekana kwake kumefuta tetesi nyingi kuwa ama amekufa kwa kujinyonga au kwa mateso akiwa gerezani. Ndugu zake walikuwa wanadai kuwa wanazo taarifa za kifo chake lakini maafisa wa magereza tangu juzi wamekuwa wakikanusha. Mchambuzi mmoja amesema, magereza hawakuwa na sababu ya kukanusha kwa maneno, wangeweza kumuonyesha anayedaiwa kufa ili ndugu zake waamini pasipo shaka

No comments:

Post a Comment