Friday, February 27, 2009

Dowans Sasa Dondandugu

Picha inaonyesha mitambo ya Dowans inayomezewa mate na Tanesco ikiwa eneo la Ubungo

Tujiulize

Gumzo la Richmond-Dowans linazidi kukua. Lilianza kama chembe ndogo ya aladani, likazidi uzito, maji yakazidi unga na vigogo watatu wakang'oka. Hadithi haikuisha, mkataba ukafutwa, Dowans ikakimbilia makamani na miktambo ikashikiliwa na Tanesco ili wakishinda kesi mitambo ifidie hasara.

Kabla kesi haijaiva, tanesco wameshadadia kununua mitambo kuukuu wanayoshikilia, licha ya sheria ya manunuzi kutoruhusu. Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja anatetea kuwa huo si ufisadi.

Kwa upande mwingine, serikali kupitia shirika lake la Tanesco imelitega bunge na kulitaka libariki mpango wa kununua mitambo hiyo, jambo ambalo limewagawa wabunge wa kamati mbili tofauti kama wanavyosema Zitto Kabwe na Dk Harrison Mwakyembe.

Lakini mambo hayakuishia hapo, tayari bunge limeshtukia mpango wa serikali na kuhoji kwanini lishirikishwe kununua mitambo hiyo wakati haijawahi kutoke likashirikishwa katika ununuzi wa vitu vingine kama magari, Katibu wa Bunge anamaliza kila kitu dhidi ya mpango huo wa wizara.

(Msimamo wako piga kura kwenye kipimajoto hapo kulia)

No comments:

Post a Comment