Thursday, February 26, 2009

CUF ni Wale Wale

Wapendwa wanahabari,

Kwa heshima tuna furaha ya kuwaarifu kuwa uchaguzi mkuu wa Chama chetu kwa ngazi ya uwenyekiti, umakamo mwenyekiti na ukatibu mkuu Taifa umemalizika hivi punde tu katika ukumbi wa Diamond Jubilee.

Wajumbe waliopiga kura ni 669 na washindi katika uchaguzi huo ni kama ifuatavyo:

i. Nafasi ya Katibu Mkuu imebakia kwa Maalim Seif Sharif Hamad aliyepata kura 651 sawa na 99.5%

ii. Nafasi ya Makamo Mwenyekiti imebakia kwa Mhe. Machano Khamis Ali aliyepata kura 644 sawa na 98.6%

iii. Nafasi ya Uwenyekiti imekwenda kwa Profesa Ibrahim Lipumba aliyepata kura 646 sawa na 97.4%.

Picha za tukio zima la upigaji kura, kuhisabu na kutangazwa kwa matokeo zinapatikana kwenye http://flickr.com/photos/hakinaumma/.

Pamoja na salamu za ChamaImetolewa na Dawati la Mahusiano na Vyombo vya Habari

The Civic United Front (CUF - Chama cha Wananchi)

No comments:

Post a Comment