Friday, January 09, 2009

Karugendo Apinga Kutimuliwa


Baada ya kufukuzwa upadri na kuondolewa kiapo cha useja (yaani kuruhusiwa kuoa), Padri Privatus Karugendo amepinga uamuzi huo kuwa si halali kwa kuwa hakusikilizwa. Haya ni maandishi yake:

" Ndiyo maana mimi ninasema kwamba, hukumu ya kesi yangu hata ikitolewa na Baba Mtakatifu, kama hajanipatia nafasi ya kusikilizwa na kujitetea, sitaikubali. Hata kama hukumu hiyo itatolewa na Mungu mwenyewe, bila kupewa nafasi ya kusikilizwa na kujitetea, nitakataa! Ninajua adhabu ya Mungu, itakuwa ni kuitoa roho yangu! Niko tayari kwa hilo! Nasimama bila kutetereka kutetea imani yangu na wito wangu. Aluta Continua! aliyoandika katika gazeti la Raia Mwema. Yasome HAPA kwa urefu.

No comments:

Post a Comment