Thursday, June 12, 2008

Bajeti Hii Hapa


Sasa unaweza kuisoma mwenyewe BAJETI YA SERIKALI 2008/09.
Kwa ufupi tu, sigara, bia, pombe kali, usajili wa magari, vimeongezwa kodi. Pembejeo za kilimo, matrekta yamefutiwa. Hakutakuwa na ongezeko la kodi kwenye petroli.
Na Kastory haka katakupa picha nyingine
Mishahara minono kodi juu

Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imefanya marekebisho katika mfumo wa kodi binafsi ya mapato na mapato ya ajira ambapo wanaolipwa kima cha chini wataendelea kutolipa kodi wakati wale wenye mishahara minono watalipa kodi zaidi.
Akiwasilisha mapendekezo ya serikali kuhusu makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka 2008/2009 bungeni jana, Waziri wa fedha na Uchumi, Mustapha Mkulo alisema lengo la hatua hiyo ni kuzingatia ongezeko la kima cha chini cha mshahara serikalini, na kulinda mapato ya ajira dhidi ya athari za mfumuko wa bei.

No comments:

Post a Comment