Tuesday, March 11, 2008

Makaburi mengine balaa


Kaburi kwa sura ya gari. Hii ni zawadi ya Marehemu Joely Kivelege aliyezikwa Kinondoni Dar es Sa Salaam, aliyopewa na Mzungu mmoja aliyekuwa mlezi wa kituo cha watoto yatima. Kivelege alikuwa miongoni mwa watoto hao. Mzungu huyo alimpenda sana kutokana na tabia yake njema. Alipotaka kwenda Ulaya likizo, alimuahidi kijana huyo zawadi ya gari, lakini aliporudi, alikuta mambo yameharibika. Kivelege alikuwa amefariki kwa malaria iliyopanda kichwani. Ahadi ni deni, mzungu huyo aliamua kumjengea kaburi mfano wa gari na hiyo ikawa ndiyo zawadi yake.

3 comments:

SIMON KITURURU said...

Ama kweli Ahadi ni deni!

Bwaya said...

Hii kweli kali. du!

Egidio Ndabagoye said...

Ebwana dah!

Post a Comment