Tuesday, February 26, 2008

Wapinzani Wavyopoteza Kiteto

WanaCCM wakishangilai ushindio wa Benedict ole Nangaro kuwa Mbunge wa Kiteto


Mwanzoni Chadema walishani mgombea wao, Victor Kimesera ndio ameshinda baada ya kuona matokeo ya mjini Kibaya, lakini kumbe, mambo yakawa kama Kenya...Kibaki (Nangaro) kaitangazwa mshindi Odinga (Kimesera) Mhh!.


FFU walikuwa kibao. Taarifa zilisema walikuwa zaidi ya 500. wote wilaya moja, kufanya kazi gani? au walikuwa wanapiga kura?


Kapteni John Komba wa TOT na Mbunge wa Mbinga Magharibi akishuka kkwenye chopa ambayo ilitumika kama silaha ya msaada baada ya Bendi yake kushindwa kufua dafu kuwashawishi watu wa Kiteto


Wapiga kura wakiangalia majina yao kwenye daftari (karatasi) za kudumu za wapiga kura. Inasemekana zaidi ya nusu ya wapiga kura hawakuona majina yao. Wengine yalikuwa kwenye vituo vya mbali na walipotarajia...Baadhi sijui wa chama gani walihamishwa kwa magari kwenda kupiga kura mbali majina yao yalipopelekwa.

No comments:

Post a Comment