Sunday, November 13, 2005

Nyerere Amwandikia Kikwete

Jokes, kampeni au kitu gani? Ebu soma BARUA HII. Nimeletewa na rafiki yangu katika mtandao, kuwa imetoka kwa Mwalimu Julius K. Nyerere kwenda kwa Jakaya Kikwete.

10 comments:

Anonymous said...

Ghafla Mwalimu Kasahau Kiswahili!

Boniphace Makene said...

Nimesoma hiyo Reginald, inatoa mwangaza kama huyo Rais atakubali kufuatialia hayo. Amesahau kusema tu kuwa Mfalme Mkapa aliyemnadi kwetu ametudondosha na kujali wageni zaidi yetu wenye nchi. Ametuuza na sasa kuna kazi kubwa ya kurejesha waliyouza.

mloyi said...

Kumbe hata peponi hatuwezi kukaa wenyewe mpaka tuwakaribishe wazungu?

Ndesanjo Macha said...

Kuhusu Mwalimu kusahau Kiswahili na kumwandikia Kikwete kwa kimombo:
Jibu: Kwakuwa tunaambiwa kuwa shetani ni mweusi na shetani wakati mtoto wa mungu (yesu) na malaika ni weupe, huenda basi lugha inayotumika huko wanakokwenda waliofariki ni kiingereza.

Anonymous said...

Bwana Miruko, leo ngoja nitoe dukuduku langu...mwenzio kila nikikutembelea lazima nisome..yale kuhusu wewe "About Me". Napenda jinsi ulivyoanza sentensi.."Yote Maisha." Bado natangatanga ......, basi maneno haya na ile picha na kalamu, kwangu mimi hutafsiri mambo mengi sana, kwamba una hasira na maisha, una hasira na watu fulani fulani, na vinginevyo vingi...Na kama siku hiyo ikijaaliwa kufika!! basi akina sisi tutakujua wewe ni nani.
Kweli uongo?

Da'Mija.

Ndesanjo Macha said...

Mzima lakini? Umekua kimya mno.

mloyi said...

Nadhani Nyerere alikukataza kutuma hii habari,nawe ukatuma kijeuri! ona sasa amekupiga tafrani hata kuandika zaidi umeshindwa.

Anonymous said...

Kwi! Kwi! Kwi! wee! Mloyi hebu acha kutuvunja mbavu....Teh! teh!teh!...

Reginald S. Miruko said...

Hapana Mloy, si Nyerere. Nilipotea kidogo kwa muda kutokana na tatizo la kusambaa kwa kasi ndogo kwa teknolojia hii. Nilikuwa mahali ambapo sikuwa na uwezo wa kupata huduma hii. Nakushukuruni wote mlioendelea kuniunga mkono na kutembelea blogu yangu katika kipindi ambacho sikuwa naonekana.RSM

mark msaki said...

labda hapa bwana da mija - anoymous kuna kaduku duku alika elezea kuhusu fasihi za bwana miruko na matazamio yake! nadhani bwana miruko anawakilisha sehemu kubwa ya umma wa watanzania ambao kwa namna moja au nyingine wanakandamizwa au kuzuiliwa japo kama sio kutoheshimiwa haki zao kama binadamu!

huyu bwana nimemtembelea sana bloguni, sidhani kwamba ana nia ya kukomoa raia wema, ila ninadhani kuwa ameishahisi nini maana ya uhuru na anatafuta ukombozi au uhuru wake! mbona watumwa tuko wengi tu tanzania?

cheers!

Post a Comment