Thursday, February 07, 2008

Kipanya na Lowassa

Waziri Mkuu, Edward Lowassa ameamua kufuata ushauri wa katuni ya Kipanya ya leo, kwamba hatamkimbiza aliyemvua nguo zake, badala yake ameamua kuchuchumaa. Hivyo amemuandikia barua Rais wake, JK kuomba kujiuzulu. Bila shaka JK atasikiliza kilio cha Watanzania wengi na kukubali ombi la Lowassa. Kwa maana hiyo Barza la Mawaziri litavunjwa na Waziri Mkuu mpya kutangazwa nadhani kati ya leo na kesho, na litaundwa Baraza Jipya. Ombi langi baraza jipya lisiwe na mafisadi.

No comments:

Post a Comment