Monday, May 29, 2006

Tanzania Karne ya 21: Bado Kuna Mumiani!

Mama huyu mkazi wa Nkuhungu Mjini Dodoma akiwa hoi nyumbani kwake, baada ya kushambuliwa na wananchi 'wenye hasira' kwa madai kuwa mumewe ni mnyonya damu (Mumiani). Mbali na kumpiga hadi kuzimia, mali zote ndani ya nyumba ziliporwa. Wamelazimika kuuza nyumba na kuhamia kusikojulikana.

3 comments:

Anonymous said...

Tuna kazi kubwa sana ya kuelimisha jamii dhidi ya fikra potovu, hivyo damu sasa hivi bila kupimwa ni dili kweli?hivi ndivyo vijiji ambavyo ikionekana gari kila mtu anakimbilia ndani akidhani ni mumuani, naomba mbunge wao aitishe vikao kuwaelimisha vinginevyo maujaji yatakuwa mengi kwa kuogopa mumiani.

Jeff Msangi said...

Miruko,
Serikali ipo wapi??Hiyo kasi mpya inamaanisha kasi ya kudunda wananchi nini?

Anonymous said...

Mbunge wao anaishi Dar-es-salaam, na huenda huko wakati uchaguzi ukikaribia. Hao waharifu waliompiga huyo mama wanatakiwa watafutwe na watiwe nguvuni mara moja ili haki itendeke.

Post a Comment