Monday, May 29, 2006

Tanzania Karne ya 21: Bado Kuna Mumiani!

Mama huyu mkazi wa Nkuhungu Mjini Dodoma akiwa hoi nyumbani kwake, baada ya kushambuliwa na wananchi 'wenye hasira' kwa madai kuwa mumewe ni mnyonya damu (Mumiani). Mbali na kumpiga hadi kuzimia, mali zote ndani ya nyumba ziliporwa. Wamelazimika kuuza nyumba na kuhamia kusikojulikana.

5 comments:

zemarcopolo said...

watanzania kiutaniutani ila tunakoelekea sio kuzuri.mbona hivi vitendo visivyoelezeka kasi yake imekuwa kali ghafla!!!madhara ya ari kama hizi ni kwamba adui zetu wakigundua tu kuna walio tayari na moyo wa aina hii,wanaweza kutumia kama mwanya wa kuchochea vita ya wenyewe kwa wenyewe.mwananchi fungua jicho!

Anonymous said...

Tuna kazi kubwa sana ya kuelimisha jamii dhidi ya fikra potovu, hivyo damu sasa hivi bila kupimwa ni dili kweli?hivi ndivyo vijiji ambavyo ikionekana gari kila mtu anakimbilia ndani akidhani ni mumuani, naomba mbunge wao aitishe vikao kuwaelimisha vinginevyo maujaji yatakuwa mengi kwa kuogopa mumiani.

Jeff Msangi said...

Miruko,
Serikali ipo wapi??Hiyo kasi mpya inamaanisha kasi ya kudunda wananchi nini?

Anonymous said...

Mbunge wao anaishi Dar-es-salaam, na huenda huko wakati uchaguzi ukikaribia. Hao waharifu waliompiga huyo mama wanatakiwa watafutwe na watiwe nguvuni mara moja ili haki itendeke.

Sufa said...

Mwalimu alisema tukimbie wakati wengine wanatembea, lakini inaonekana Mwalimu alikuwa karne kadhaa mbele kwani wengine bado wanasota. Tunakazi mbele yetu tena kubwa mno.

Post a Comment