Wednesday, January 11, 2006

Tunazipenda Alama za Taifa?

Wakati wa Kampeni za Urais zilizopita ulizuka mjadala mrefu wa ama Freeman Mbowe, mgombea wa Chadema anaruhusiwa kuweka bendera ya Taifa kwenye mabango yake ya kampeni au la. Tume ya Uchaguzi, kwa kutumia sheria zilizopo, ilimpiga marufuku kuitumia bendera hiyo, lakini yeye aliibishia na hakuiondoa.

Baada ya uchaguzi, Rais Jakaya Kikwete ametangaza kuanzisha mjadala wa kitaifa juu ya kuhamasisha Watanzania wazipende na wawe huru kutumia alama za Taifa ili kujenga ari ya kuipenda nchi yao. Hali hiyo bila shaka itaondoa sheria za 'kipumbavu' za kuzuia Mtanzania kuwa na bendera ya nchi yake, lakini akaruhusiwa kuwa na marekani. Zikiruhusiwa mimi nitatundika nembo hii ya taifa(juu kushoto) ndani kwangu, wewe je?. -RSM-

3 comments:

FOSEWERD Initiatives said...

nitaweka na jinsi JK anavyonifurahisha wala sisiti kuutangazia umma kuwa mimi ni mtanzania halisi tofauti na mawazo yangu hapo nyuma kidogo!

Ndesanjo Macha said...

Kinachonishangaza kuhusu Kikwete ni kuwa mambo mengi yaliyokuwa yakilalamikiwa wakati wa uchaguzi, yeye hakusema lolote. Sasa baada ya kuchaguliwa ndio anasema nembo za taifa zitumiwe, muungano ujadiliwe, takrima ijadiliwe, ruzuku za kampeni, n.k. Najua kwanini hakuwa anaongelea haya mambo wakati wa kampeni. Sipendi kabisa mwanasiasa ambaye ana msimamo kutokana na upepo na sio kanuni alizozishika bila kujali upepo. Tabia hii ndio inafanya watu wengi kusema siasa ni mchezo mchafu. Sio lazima uwe mchezo mchafu. Tunaweza kuwa mchezo msafi iwapo tutakuwa wa kweli, wenye kufuata maadili na kanuni bila kujali upepo.

FOSEWERD Initiatives said...

ndesanjo, nina wasiwasi pengine angekuwa mkali hapo nyuma asingekatiza. hata hivyo hakuna anayejua. cha maana ni kuwa tunahitaji kuwa na taasisi imara za kusimamia masuala ya mustakabali wa taifa na si wanasiasa.

Post a Comment