Wednesday, January 11, 2006

Hii Ndiyo Kasi Mpya

Kasi Mpya ya utawala wa Rais Jakaya Kikwete imeanza kuonekana rasmi. Waziri wake mpya wa Usalama wa Raia, Harith Bakari Mwapachu ameweka mambo hadharani kwamba 'Majambazi yanayoua lazima nayo yauawe'. Natambua wazi kuwa TAMKO HILI la waziri litapokelewa vizuri na Watanzania wengi wanaokerwa na majambazi, lakini litapingwa sana na wanaharakati wa Haki za Binadamu. Sijui nani atakuwa na haki ya kulikubali au kulipinga.-RSM-

1 comment:

mark msaki said...

mimi ninamuunga mkono. nilimwelewa vyema waziri akiwa na maana kuwa kama jambazi ameenda eneo la tukio na smg na anamimina marisasi basi bolisi naye amimine za kwake....sio kwamba akamatwe halafu ahukumiwe kifo!

Post a Comment