Friday, January 20, 2006

Njaa Kali Kwa Kasi Mpya


HAPA Tanzania ukitamka kuwa kuna njaa, viongozi wanabisha, wanadai kuna upungufu wa chakula. Sijui kilichopo sasa kati ya haya mawili, lakini hali halisi ni kwamba watu hawana chakula, na mifugo haina malisho wala maji ya kunywa. Picha za Mpoki Bukuku wa The Citizen, zinajieleza.

7 comments:

boniphace said...

Kaka hizo picha ziko wapi tena. Tuwekee tutazame nasi tujue ukweli.

mwandani said...

Njaa inatokana na upungufu wa chakula au kutokuwepo kabisa chakula.Hoja inayobainisha misamiati ya njaa na upungufu wa chakula sidhani kama vitaondoa tatizo.
Hivi unajua kama kuna mikakati ya matayarisho ya kuepusha njaa au upungufu wa chakula (disaster preparedness na mitigation)? Maana balaa la njaa linashukia taratibu sio kama balaa la tsunami ya papo kwa papo. Naomba utupe kidogo zaidi juu ya suala hili.

nyembo said...

ni asubuhi,saa ukutani inanijulisha kuwa yapata saa moja kamili za wakati huo, kikombe cha kahawa mkononi nasikila kwa makini redio ya mwafrika mwenzangu Anthony DialloRadio Afrika Huru (RFA) iko Mwanza kule mimi nasikiliza mkebe wangu tu! nao nauita Radio pia, namsikia Mtangazaji anatangaza "Uji wa ubuyu wauwa watu wawili" wa familia moja huko sehemu za pwani ya kusini ya bahari ya Hindi katika Tanzania,ni kutokana na kukosa Chakula, Jeshi la Polisi linasema kuwa wao hupokea Taarifa ya vifo tu na sio taarifa ya njaa au watu kukosa chakula....
sijui kuna tatizo gani kwa Jeshi ama Serikali kuukubali ukweli wa chanzo cha tatizo kuwa ni njaa?

Christian Bwaya said...

Miruko,
Njaa mwaka huu ni tishio. Nimesoma gazeti mla mwananchi, Singida watu wanaponea mizoga! Mifugo inapukutika. Nashangaa sana wanasiasa wanatangaza kwa kujiamini kabisa kuwa hakuna njaa na kwamba hakuna mwananchi atakufa kwa njaa!
Mimi nashindwa kuelewa, hivi hizi kauli zinatoka wapi wakati nchi nzima hakuna mvua?
Kuna tatizo ambalo nashindwa kulielewa kimsingi: hii tabia ya kukanusha mambo ambayo yako wazi.
Sirikali (hata kama haipendi kusikia habari ya njaa)inapaswa kuchukua hatua za haraka sana (hata kama ni kisirisiri) kuwanusuru wananchi. Kipaumbele kielekezwe kwenye chakula na sio vinginevyo.

FOSEWERD Initiatives said...

hiyo ni kali!! mwandani umenigusa maeneo yangu ya kujidai....hoja ya muhimu sana uliyoitoa! kuna haja sasa kuacha kufanya kazi kama zimamoto!

boniphace said...

Miruko tuanikie ukweli maana umekaa kimya sana. Hizo picha niliomba hukutuwekea lakini tunasikia tu kuwa njaa sasa ni kwa kasi mpya na kila jambo sasa ni kasi mpya nini hasa maana ya haya maneno huko Tanzania. Na hapo Dodoma ndipo maeneo hasa nasikia watu wanashindia zabibu hii kauli ni ya kweli?

Reggy's said...

sorry, nilikimbia njaa kidogo, nikaenda dar ambapo njaa inaonekana tu kwa vyakaula kupanda bei. Mfano mzuri, ni unga wa sembe/dona umepanda kutoka sh 300 hadi sh 500. akini yaliyopo Dodoma ni haya hapa.

Post a Comment