Sunday, February 05, 2006

Mfalme Mswati Anaonewa Wivu?

Hawa ni baadhi ya vibinti' (vigori) ambavyo Mfalme Mswati wa Uswaz, hutakiwa kuchagua mke wake moja kila mwaka. Sasa hivi anao 14. Dunia inalaani kitendo chake ambacho, hata hivyo, ni utamaduni wa nchi hiyo. Je Dunia inamuonea wivu?mwati 3

8 comments:

mwandani said...

haki hii ya mfalme mswatiii... Duh!
Naona ana supply kubwa sana, kimaadili sipendi utaratibu wa kutongozewa na kupata mwali kama zawadi, sitaki kuwa msemaji wa haki za kina mama kwa sasa ila naona ni vizuri ndoa iwe kwa ridhaa na makubaliano ya wapendanao, kwa upande mwingine nimewakodolea na nimewapeleleza hao kina dada pichani kwa makini sana, sina wivu lakini udhaifu wangu unanishinda nguvu na mawazo yanaelekea nisikotaka... Watu weusi ni warembo sana, sijui unanipata?

John Mwaipopo said...

Mwandani umenena mambo mengi mema kwa aya chache tu. Hongera.

Miruko: Wazungu wa nchi za magharibi wamegubikwa na wivu tu. Ninachokifikiria hapa ni kuwa iwapo hawa vigori hawajalazimishwa na mtu yeyote kujiparade namna hiyo basi dole tupu. Kama ni vinginevyo basi nina mawazo tofati kidogo. Kilichopo duniani sasa kwa sababu ya 'utandawizi' ni kuwa kila kinachosemwa na watu wa magharibi kinaonekana ni chema. yawezekana kwa sababu kinasemwa kwa kingereza. Upuzi mtupu! Wamwache Mfalme Mswaki, sorry Mswati, na utamaduni wa watu wake.

Reginald S. Miruko said...

Ninakupata vilivyo bwana Mwandani, waafrika wana maumbo mazuri, japo, kama alivyosema dada Chemponda, kuna tatizo la kupenda matako makubwa tanzama hapa, http://swahilitime.blogspot.com

Jeff Msangi said...

Hivi lipi bora,kuwa na wake 14 wa halali na wanaotambulika kote au kuwa na mahawara (nyumba ndogo)20?

mark msaki said...

kwani na sisi nani katuzuia? mbona hata babu zetu waliotukuka kimaadili ya dini walikuwa wanafanya mambo (kuwa na wake kadhaa)? mbona hata hao bibi zetu walikuwa na raha sana na maisha ilikuwa inaenda vyema tofauti na sasa??? ni lini vitabu vitukufu viliingilia kati na kusema mke ni mmoja tu? si ndio wazungu walituweka kwenye line? matokeo yake na walivyotuletea ukimya (ukimwi) hatuna ujanja tena (rejea point ya Jeff)!! mbona ukimwi hauwawezi waarabu lakini sisi tunapotea?? huu mjadala nimeupenda, siku moja nitatoka nao rasmi!

ndesanjo said...

Kwa mujibu wa kitabu "kitakatifu" ambacho wengi wanakiamini ingawa hawakisomi, yaani biblia, Mfalume Suleimani alikuwa na wake mabibi 1000. Yaani wake na nyumba ndogo changanya.

Piga mahesabu: mwaka una siku 365 hivi, wake anao 1000...sema mwenyewe.

Anonymous said...

kwa kweli mimi mwenyewe japo nimeokoka, bado nawashangaa wazungu!! Wanataka tujikatae completely na tuwe kama wao japo MUNGU alituumba jinsi tulivyo??
Watu weusi tukiendelea kuamini kila kinachotoka kwa wazungu maana yake ni kwamba inamaanisha MUNGU hawezi kusema nasi na kuishi kama anavyopenda yeye(MUNGU)!!

Anonymous said...

FEREFERE...
mflalme mswati anadumisha mila swaz tutambue kila nchi ina utamaduni sasa inchi za magharibi naona zinataka tamaduni zao ndizo zifuatwe kwa kila nchi sasa inatakiwa nao wafike mahala watambue na waheshimu tamaduni za nchi zingine.

Post a Comment