Wednesday, January 04, 2006

BARAZA LA KIKWETE

Rais Jakaya Kikwete amewateua wafyatao kuwa mawaziri. Mnawaonaeje?

1. Zakia Meghji Waziri wa Fedha,
2. Dk.Asha Rose-Migiro Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa
3. Anthony Diallo Waziri wa Maliasili na Utalii
4 Stephen Wassira Waziri wa Maji
5. Margareth Sitta Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi
6. Andrew Chenge Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
7. Mzee Kingunge Ngombale-Mwiru Waziri Nchi Ofisi ya Rais, Siasa na Uhusiano wa Jamii
8. Phillip Marmo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Utawala Bora)
9. Hawa Abdlahaman Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejiment na Utumishi
10.Dk. Hussein Mwinyi, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano)
11.Prof Mark Mwandosya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (mazingira)
12.Profesa Juma Kapuya Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
13.Prof. David Mwakyusa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
14.Joseph Mungai kuwa Waziri wa Kilimo Chakula na Ushirika
15.Nazir Mustafa Karamagi Waziri wa Viwanda na Biashara
16.Prof. Peter Msola Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu
17.Basil Mramba Waziri wa Maendeleo ya Miundombinu
18.John Magufuli Waziri wa Nyumba na Maendeleo ya Makazi
19.Prof. Jumanne Maghembe Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana
20.Mohammed Seif Khatibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo
21.Bakari Mwapachu Waziri wa Usalama wa Raia
22.John Chiligati Waziri wa Mambo ya Ndani.
23.Juma Akukweti Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Bunge)
24. Mizengo Pinda waziri ofisi ya waziri mkuu (TAMISEMI)
25. Dk. Juma Ngasongwa Waziri wa Mipango, Uchumi na Uwezeshaji
26.Joseph Mungai Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika
27.Dk. Mary Nagu Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba
28. Dk. Shukuru Kawambwa waziri wa Maendeleo ya Mifugo
29.Dk Ibrahim Msabaha Waziri wa Nishati na Madini
BARAZA Lenyewe hili hapa

2 comments:

FOSEWERD Initiatives said...

kwa kweli bado nalitafakari...

haraka haraka naona huyu mheshimiwa ameweka baraza lenye mguso - yaani lenye kujibu mahitaji kwa maana ya majukumu.'

pia ameonekana kuwa ana nia nzuri ya kumsimamisha mwanamama kwa uraisi baadae ikiwa tu ile kitu ya EAC haitaingilia.

ana maprofesa wa kutosha kumshauri kwa ukaribu, kama hawataharibikiwa. hawa watamuunganisha na wasomi kujua ipi njia bora ya kukatiza. - tatizo moja la viongozi wa bongo wamekuwa hawawasikilizi wasomi wao.

kingunge nae? sijui hiyo wizara inataka busara, lakini sijui kama atasahau kufagilia chama cha mapinduzi na kuwa wa waziri wa wote!!

katenga usalama wa raia na polisi! maana polisi walijidai kuwa wana uwezo wa kunyanyasa umma kwa gia ya kuwalinda!

hii wizara mpya - kazi, ajira na maendeleo ya vijana imenichengua na kuna profesa pale juu!!! mtumeee hakuna kisingizio cha kushindwa!!

maendeleo ya miundo mbinu!! yaani ndio barabara, maji, viwanja vya ndege! bora asituhamishie kwenye kula udongo. bora atubakize kwenye kula nyasi tu!!

mungai tena! mh hapo sina la kusema!

afya na ustawi wa jamii - imekaa vizuri maana watu wanakufa kukosa 500 ya matibabu!!

kwa marmo nadhani ndio penyewe!

wassira spephen - huyu huitwa boxer. ni mtu serious. sijui bado yu hivyo siku hizi.

diallo ni mwekezaji. naona pale panamfaa ili anyanyue uwekezaji maliasili na utalii.

meghji akacheze na TRA. nasikia utalii umepanda chati miaka ya karibuni! awe mkali zaidi ila. tunataka kila duka liwe na till iliyoungwa kwenyue computer za TRA. na kuwe na shopping malls kila mkoa, haya mambo ya kutandaza vibox kila sehemu hatufagilii!!

chenge sawa pale panahitaji mwanasheria.

hii jkt wanataka kuirudisha iharibu vijana wetu zaidi au ?????

hii cv ya kamaragi wa viwanda na biashara ni ya kufuatilia zaidi.

kweli huyu bwana hatabiriki. kuna sura mpya humu. tusubiri.

FOSEWERD Initiatives said...

pole sana bwana miruko. naona unavuta pumzi baada ya mchaka mchaka mzito wa kutuletea live toka viwanja vya makao makuu. mungu akutie nguvu urudi kwa kasi kasirini!

Post a Comment