Nitakuwa wa mtu ajabu nisipoeleza yaliyojiri baada ya Rais Jakaya Kikwete kumteua Edward Lowassa kuwa Waziri Mkuu wa Tanzania. Mambo yenyewe ni haya:
1. Alithibitishwa kwa kura za NDIYO za wabunge kwa asilimia 99, wawili tu walimpigia kura za HAPANA.
2. Mbali na wabunge wa chama chake, CCM, Kambi ya Upinzani bungeni ilimkubali kuwa ni mchapakazi, mwenye uzoefu wa kutosha, lakini wakaonya asijali maslahi ya CCM, bali maslahi ya taifa.
3. Wengi walisema walitarajia hilo kwa kuwa Kikwete ni Raifiki wa karibu na Lowassa, na waliwekea mkataba kuwa amuachie urais yeye atapewa U-PM.
4. Baadhi walidhani Kikwete atamuacha kwanza, amchukue baadaye, kwa kuwa aliwahi kukanusha kuwa na baraza la Mawaziri mfukoni hata kabla ya uteuzi wake, lenye sura za Lowassa na Rostam Aziz (marafiki zake). Hayo yalitokea pale alipoulizwa swali wakati wa kuchukua fomu za kuwania Urais kupitia CCM
5. Mimi binafsi naamini kazi kubwa iliyofanyika kwa Lowassa na Kikwete, ni ya vyombo vya habari. Viliwapamba kwa miaka 10 na kukandamiza washindani wao kwa miaka 10
6. Kikwte amemtetea katika hotuba yake 'kali' kwa wabunge kuwa hakumteua Lowassa kwa urafiki, bali kwa utendaji wake. -RSM-
No comments:
Post a Comment