Wednesday, December 28, 2005

SPIKA MPYA AWAPA ONYO MAWAZIRI

SPIKA mpwa wa Bunge la Jasmhuri ya Tanzania, Samwel Sitta ameanza kazi kwa kutoa onyo kali kwa mawaziri watakaoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete.

Amesema, " Natoa onyo kwa Mawaziri watakaoteuliwa katika serikali hii kuwa majibu yasiyotoa ufumbuzi wa matatizo ya wananchi hayatakiwi. Nitaomba Bunge liniunge mkono ili tusiwe na uvumilivu wa Mawaziri wa namna wanaotoa majibu yasiyo na ufumbuzi wa matatizo ya wananchi," (mwisho wa kunukuu).

Katika mchakato wa Chama Tawala, CCM, Sitta alimshinda kwa mbali Spika wa zamani, Pius Msekwa na katika Uchaguzi wenye wa Spika, alikuwa mgombea pekee na kupita bila kupigiwa kura. Mgombea wa Chama cha National League for Democracy (NLD),Ascetic Malagila, alijitoa kwa madai kuwa Sitta anakubalika.

Sitta aliwahi kuwa Waziri wa Sheria miaka ya nyuma na alikuwa Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC). Kwa sasa ni Mbunge wa Jimbo la Urambo mkoani Tabora-RSM-

11 comments:

Anonymous said...

Kama si mbwembwe na bashasha la ushindi basi msimamo wa spika mpya, Mheshimiwa 6, ndio tunaoutaka. Majibu ya ubabaishaji ambayo hata mimi siwezi kuyatoa yasiwe na nafasi kamwe katika bunge letu.

Kwa mfano, katu sitaweza kusahau jibu la ubabaishaji lililowahi kutolewa na mheshimiwa Mary Nagu alipokuwa-ga waziri wa wanawake na watoto. Swali lilikuwa serikali ilikuwa na mpango gani na nguo fupi zilizokuwa maarufu kwa dada zetu. Yeye akajibu "mbona hata wanaume wanavaa nguo za nusu uchi".

Kukiwa kuna ukweli kuwa wanaume nao si hapba katika mavazi lakini hakujibu swali aliloulizwa.

Anonymous said...

Nimesikia tetesi waziri mkuu aweza kuwa Anna Abdallah. Miruko unasemaje?

Da'Mija.

boniphace said...

Mwaipopo umefufuka lakini kilio chetu ndugu yangu ni hilo blogu lako linakuja lini? Tumechoka kuungana nawe kwenye kuchangia mijadala tu ebu leta hilo blogu haraka.

Ok msimamo huo tunasubiri nadhani nimefafanua pia hili katika Kasri, tunangoja huyu Waziri Mkuu Mwanamke, Anna Abdallah hawezi kuwa Waziri Mkuu kwa kuwa ni mbunge wakuteuliwa hivyo Da Mija futa kabisa utabiri huo labda mtaje taje MONGELA.

FOSEWERD Initiatives said...

mie kwanza niwapongeze wabunge kwa uamuzi waliochukua. kwanza kupunguza watu wanaofikiria wana copyright (hatimiliki ya Tanzania)na pili kutumia haki yao ya demokrasia bila kuangalia makunyanzi.

mrejesho nyuma wa mh. sitta nadhani unanipa matumaini. kwanza ni mwanasheria. halafu kile kiitengo alichoongoza cha uwekezaji kimempa uwezo wa kuongoza bunge lililo na uelewa mkubwa juu ya utandawazi na nafasi ya watanzania katika uwekezaji. ninaamini pia teyari anawafahamu wawekezaji wako wapi' na wanataka nini. nipepeda kauli yake pia kuwa bunge sio sehemu ya kwenda likizo kwa mawaziri.

ninashukuru pia kikwete atafanya kazi na macolleague wake ambayo ni bora kuliko mzazi wake.


jamani msipende kuteua waziri mkuu kutokana na majina. naomba tuteue kutokana na kazi na uwezo wa kukimbia mchakamchaka kiutendaji uwezo wa kukabiliana na mstari mfu katika utendaji. pia awe mzalendo. je ni nani ambaye muhishimiwa Kikwete akimpa ile kauli mbiu iliyompa ukuu anaweza kuiimplement? kubuka tunataka waziri mkuu ambaye atatekeleza ahadi zaidi ya milioni katika juhudi ya kuleta maisha bora kwa kila mtanzania tena kwa kasi mpya, ari mpya na nguvu mpya. mimi nina watu wawili ninawafikiria wa kwanza ni mheshimiwa lowassa na wa pili ni magufuli. hakuna ubishi kwa hili. lowasa aliwavimbia wamisri ili apeleke maji shinyanga na kidogo zingechapwa. nina uhakika walishataka kumuona kwa akaunti yake waarabu hawa akadinda. magufuli tumemuona jinsi alivyomwaga mikeka na ile syle yake ya mrema mrema.

cheers

Anonymous said...

Sawa Makene nimefuta, sasa naanza kutaja taja Mongella.

Mungu saidia utabiri wangu.

Da' Mija.

FOSEWERD Initiatives said...

bwana miruko,

tunasubiri habari mvunjo kuhusu nani ni waziri mkuu!

jamani kwa wale wanaomfagilia Mh. Mongela. ni nini hasa credits???? zake kiuongozi? mimi nilimfahamu zaidi kama mwanaharakati wa kina mama na mzoefu kwenye siasa za kimataifa. je tunamtaka kwa sababu tulishuhudia akionewa na kina msekwa? au kwa kuwa ni mwanamama? au ni kuwa hajapewa nafasi? ni nini zaidi ninaomba munipige shule ili na mie nimwoombe kwenye suala zima la uteuzi!

cheers

Fikrathabiti said...

Bwana miruko nakupongeza kwahilo!
Ukipata nafasi tembelea kwenye fikra zangu kwani nami tangu jana niliweka makala na leo nikaingiza fikra nyingine katika mtindo wa ushairi

Wewe unadhani falsafa aliyokuja nayo Sitta ya "THE STANDARDS AND SPEED" inaleta matumaini yoyote katika bunge letu hili tulilozoea kuwaona baadhi ya babu zetu wakiuchapa usingizi tu??!!!!!!!

Reggy's said...

njakushuruni kwa mjadala. Anna Abdallah hawezi kuwa Waziri Mkuu, kwani si mbunge wa Jimbo, kama alkivyosema Makene. Mongela hawezi pia bado wanamfagilia aendelee kuwa Spika wa Bunge la Afrika (Uchaguzi unafanyika kesho, na sasa hivi amesharejesha fomu za kuomba kuchaguliwa) na Spika, Sitta, amewataka wabunge 'wazingatie maslahi ya Taifa' katika uchaguzi huo. Anna Makinda ni Naibu Spika hadi sasa. Kimsingi sioni mwanamama mwingine. Spika anaweza kuwa Rafiki Kipenzi wa Kikwete, Lowassa au ikishindikana, Raustine Kabuzi Rwilomba wa Busanda, Geita, Mwanza.

FOSEWERD Initiatives said...

miruko,

sio spika sasa ni waziri mkuu!

macho na masikio ni kwenye blogu lako tu sasa!

cheers,

Mija Shija Sayi said...

Muziki bado ni ule ule ila vyombo ndo vimebadilishwa.

mloyi said...

Waziri mkuu kapatikana tayari! Sasa tunaongelea mawaziri- au wasaidizi wa raisi.
ijui nani atabaki na kwanini yule harudi tena sasa? Wale watabiri thibitisheni uwezo wenu wa kutabiri.

Post a Comment