Thursday, December 29, 2005

Ni Edward Lowassa?

Si lengo langu kukuulizeni maswali ninyi wasomaji wa blogu hii. Hii inatokana na ukweli kwamba mimi si Mtabiri, lakini duru za hapa bungeni Dodoma, masaa manne kabla ya uteuzi wa Waziri Mkuu zinaonyesha ni Edward Ngoyai Lowassa. Aliyezaliwa Monduli Arusha. Kasbla serikali ya Awamu ya Tatu haijamaliza muda wake alikuwa Waziri wa Maji na Maendeleo ya Mifugo.

Ni Rafiki Mkubwa wa Rais Jakaya Kikwete (Kikwete aliwahi kukiri hadharanmi nilipomuuliza wakati anachukua fomu za uteuzi wa CCM April mwaka huu), alikuwa kiongozi wa kampeni za Kikwete na miongoni mwa walioitwa na Kikwete kama 'wanamtandao' ambao kimsingi ndio waliomjenga kupitia vyombo vya habari na kampeni nyingine dhidi ya wapinzani wake. Tusubiri saa 11 jioni leo tuone.

2 comments:

mark msaki said...

nadhani pia kikwete anahitaji mtu ambaye hatamuangusha! kama ni lowasa sitalalamika sana. labda kama akitaka apelekwe mambo ya nje ili achukue serekali ijayo!

dhamana anayo kikwete. yote katika kuuhakikishia uma kuwa ile kauli mbiu yake haikuwa danganya toto! kinyume cha hapo, 2010 itabidi amfufue mwalimu aje mpigia debe

tunasubiri mavituvitu toka kwenye blogu hili la mavitivitu.

cheers

Reginald S. Miruko said...

Kweli, Ni Lowassa.

Post a Comment