Wednesday, December 28, 2005

MBUYU UMEANGUKA PWAA!

msekwaHayawi hayawi sasa yamekuwa. Utawala, udkteta, ubabe na...wa yule Spika wa Bunge wa Muda mrefu, Pius Msekwa ambaye karibu kila mtanzania anamjua yeye binafsi na sauti yake ya kuendesha bunge umefika kikomo.

Msekwa ameangushwa katika kura za wabunge wa CCM, waliompa kura 53 tu dhidi ya 217 za samwel (6) Sitta. Kwa maneno mengine ameshindwa kwa kishindo, Pwaaaa. Sishabikii sana, lakini nilikuwa naona umuhimu wa Msekwa kuwapisha vijana (waliochini ya umri wake) waongoze bunge.

Jinsi ilivyokuwa ungeweza kudhani Msekwa alizaliwa kuwa Spika tu mpaka aende kwa Nyerere. Kumbuka aliingfia bungeni kama Katibu mwaka 1962, Rais Jakaya Kikwete akiwa na umri wa miaka karibu 10, alikuwa mbunge, akawa Naibu Spika, akawa Spika kwa miaka 10, na bado alitaka kuendelea hadi alipopigwa mweleka na sanduku la kura.

Mbuyu umeanguka. Kumbuka pia kuwa ndiye alitunga Katiba ya Nchi, akatunga kanuni za bunge, akajipa madaraka ya kidkteta. sasa ameanguka. Wazee wenzie wanaodhani walizaliwa kuwa viongozi wao pekee, wajifunze. wamuulize Msekwa na rafikiye, John Malecela.

1 comment:

mark msaki said...

kaka miruko,

naomba nikushukuru kuwa wewe ndio umenifahamisha rasmi habari hii maana kila saa ninachungulia bbc hata hawajaweka. kweli blogu zidumu.

mimi kama mshabiki wa mabadiliko ninasikia raha sana, si kwamba nilimchukia mheshimiwa Msekwa lakini sikupenda jinsi alivyopiga u turn. pia ninashukuru kuwa lile kundi la watu ambalo lilidhani lina copyright ya kuongoza tanzania linapata shule ya moto sana! namna hii nadhani tutafika! na hata upinzani utapendwa sasa.

naona hata wahishimiwa wabunge walitaka kutuonyesha kuwa mambo ni tofauti na tulivyofikiri!!

mungu ibariki Tanzania,

mungu mbariki Miruko!

Post a Comment