Wednesday, November 02, 2005

Ni wizi wa kura au mazingaombwe?

Nimeamini. Haki huwezi kuipata kwenye sahani. Chama cha CUF, pamoja na kushindwa kwake visiwani Zanzibar (soma hapa) kimethibitisha mambo kadhaa. Ni chama chenye nguvu, kinapendwa na kukubalika visiwani humo. lakini pia kimeonyesha kuwa Haki haiwezi kusububiriwa mezani lazima ipiganiwe sana. Kama CUF isingekuwa ngangari kwa kupigana na CCM bega kwa bega, ama kura zingeibwa sana, au mapandikizi kwenye uchaguzi wangekuwa wengi na CCM ingependa kushinda kwa ushindi inaodai wa Tsunami.

3 comments:

Boniphace Makene said...

Reginald naona hujamaliza kisa hicho fafanua namna ya wizi huo maana huku ughaibuni tunaona aibu juu ya taarifa zinazotangazwa na mashirika ya kimataifa. Ongeza usijali maana huo ufalme wa CCM utatutumbua usaa na kusababisha machafuko na siku si nyingi kama darubini langu litazamavyo.

Reginald S. Miruko said...

Nakushukuru bwana Makene kwa kuonyesha nia ya kufahamu zaidi juu ya uchaguzi wa Zanzibar na kasheshe ya kura. Nitafafanua. -Reginald

Ndesanjo Macha said...

Kiungo hapa kina kasoro.

Post a Comment