Tuesday, November 01, 2005

Huu Ndio Ushindi wa Tsunami?

Tuliahidiwa ushindi wa Kishindo cha Tsunami katika Uchaguzi Mkuu wa Tanzania. Tanzania ni pamoja na Zanzibar, Mimi binafsi, nimeshindwa kuelewa kama huu ndio ushindi wa Tsunami tulioahidiwa na Rais wa Zanzibar Aman Karume. Mambo yanakaribia kuharibika. Hali ni tete na kila chama, kati ya CCM na CUF, kinatangaza ushindi. Waungwana mnasemaje?

No comments:

Post a Comment