Tuesday, August 23, 2005

Kikwete Aogopa Mdahalo. Why?

Rais Benjamin Mkapa ni mahiri kwa kuongea na kujenga hoja. Alionekana hivyo hata kabla hajaukwaa Urais wa Tanzania mwaka 1995, hasa pale aliposhiriki mdahalo wa wagombea Urais. Pamoja naye, wengine walikuwa Augustine Mrema (NCCR-Mageuzi), Profesa Ibrahim Lipumba (CUF) na John Cheyo (UDP). Kwa Sasa Mkapa (CCM) ni Mwenyekiti wa CCM.
Kinachonishangaza sasa ni CCM hiyo kumzuia Kikwete kushiriki mdahalo wa wagombea watano wa Urais. Wamebaki wanne; Mrema (TLP), Lipumba, Dk. Sengondo Mvungi na Freeman Mbowe (CHADEMA).
Kwa nini CCM wameamua hivyo? Wanaogopa nini? Wana wasiwasi na ujengaji hoja wa mgombea wao? au Kikwete hana cha kuwaeleza Watanzania kupitia Channel Ten?
Mimi sikubaliani nao hata kidogo.

3 comments:

Ndesanjo Macha said...

sikujua kuwa chama chake kimemzuia kushiriki kwenye mdahalo. hicho ni kiburi au nini?

Egidio Ndabagoye said...

Walikuwa hawajandaa uongo wa kutupa sisi wananchi

Rama Msangi said...

Kunya daima anakunya kuku na ndio maana kwao haiwezi kuwa issue, angekataa mtu wa upinzani nadhani CCM ingeomba mbingu zimshukie ati

Post a Comment