Wednesday, August 24, 2005

KAZi YA CCM!

Baada ya jana kuzuka taarifa rasmi kuwa CCM 'imepuuza' mwaliko wa mgombea wao wa Urais, JK kushiriki mdahalo wa Kituo cha Televisheni cha Channel Ten, matokeo yake si mazuri.
Kituo hicho kimetangaza kusitisha mdahalo huo na kuwaomba radhi wagombea wa vyama vingine vinne waliokuwa wamekubali. Hili pia silielewi. Kwani CCM isiposhiriki mdahalo hauwezi kunoga? Kwa faida ya yule alosema hakujua kama CCM imemzuia Kikwete, ilikuwa hivi: Omari Mapuri, Katibu Mwenezi wa CCM alisema: 'Chama hicho hakitakuwemo kwenye mdahalo huo, kitaendelea na ratiba yake'. Hakujibu swali why? Kwa mujibu wa raitiba hiyo, siku hiyo Kikwete atakuwa na mkutano wa hadhara mkoani Ruvuma. Yawezekana ni kiburi.

No comments:

Post a Comment