Monday, August 22, 2005

Digrii Hadi Mlangoni Poa

Digrii hadi mlangoini ndivyo inavyotakiwa kuwa. Kwa nini Mtu afunge safari kutoka Kiraracha hadi Marekani kufuata karatasi la digrii? Tena akiwa busy na kampeni?

Nani alisema lazima mtu ahudhurie mahafari na kuja na digrii yake mkoani? Posta ziliwekwa za nini? Binafsi niliwahi kuletewa Cheti cha Diploma nyumbani nilimwagiza mtu aanifuatie chuoni. Hii ni sawa na kukipata kwa fax, nongwa inakuja anapokuwa ni Mrema.

Wengine wanahoji kwenye magazeti eti Mrema amesoma kwa muda mfupi, amejikabidhi cheti na amejivalisha joho, lakini 'wakuda' hao hawahoji wanasiasa wengi wa hivyo hapa nchini, tena si tu ma-bachellor kama Mrema bali madaktari wa falsafa (PhD holders), waliosoma kwa mtandao 'au kuzinunua' na kutunukiwa digrii zao kimya kimya, ikawa usiku inakwa asubuhi, unasikia fulani ni Daktari.

Mwingine kadai eti Mrema amejivisha joho, sijui nani alimweleza kuwa graduate huvalishwa joho na mtu mwingine? Mwingine kasema eti sherehe ya Mrema haikuhudhuriwa na mwakilishi yeyote wa Chuo, sijui nani alisema kuwa wawakilishi wa vyuo huwafuata wahitimu nyumbani kusherehekea mahafali? Mwacheni Mrema wa watu afurahie digrii yake ambayo wengine, hata viongozi wa juu wanaitafuta hawaipati.

1 comment:

Indya Nkya said...

Bravo Regnald. Cha muhimu sana ni hicho ulichouliza kwamba siku hizi kuna madaktari kibao ambao hata ukiuliza wamepataje hico pihechidii huwezi kuelewa. Utasikia tuu Daktari so and so. Mzee wa Kilalacha kasoma miaka miwili kajitahidi kuna wanasiasa wamenunua digirii bila hata kufungua hicho kitabu. Mjadala wa maana ungekuwa kama kuna unajisi wa elimu kwa kupitia hizo degree ambazo watu wana wasiwasi nazo na si kumkaba mtu mmoja awe Mrema au nani. Watu wajifunze kujadili maswala badala ya kujadili watu.

Post a Comment