Saturday, July 16, 2005

Watathubutu Hawa? Hapana!

Rais aliyebakiza miezi mitatu kuiongoza Tanzania Benjamin Mkapa (Pichani juu kushoto)jana aliungana na Waziri wake machachari wa Ujenzi, John Pombe Magufuli (kulia chini) kuwa ifikapo keshokutwa vigogo wa serikali waliokopa nyumba za serikali na hawajamaliza kulipa deni, watanyanganywa nyumba hizo.
Jumapili iliyopita, Magufuli alitia wiki moja watu hao wakiwemo mawaziri, makatibu wakuu, wakurugenzi, wakuu wa miko na wilaya na vigogo wengine wanadaiwa mabilioni ya fedha za nyumba hizo. Kauli ya jana ya Rais, kuwa apelekewe majina hayo hasa wale aliowateua kwani ana uwezo wa kuwatemesha kibarua kilichosalia cha miezi mitatu na uwezo wa kuwanyanganya nyumba hizo na kuwauzia wengine. Swali linalosumbua sasa ni je, hiyo ni nguvu ya bia au ya soda?, Tusubiri tuone.

1 comment:

Indya Nkya said...

Uigizaji tuu, walionunua hizo nyumba wanajua kinachoendelea. Hakuna chochote kitakachofanyika, wanajua usanii uliotumika kuuziana hizo nyumba. We ngoja uone.

Post a Comment