Tuesday, July 12, 2005

'Utitiri wataka urais nani ataambulia nini?


Jana, pazia la kuwania Urais wa Tanzania katika awamu ya nne lilifunguliwa. Kwa mpigo, viongozi watano wa Vyama vya Upinzania, TLP, CUF, NLD, NCCR-Mageuzi na Demokrasia Makini walijitosa kichwakichwa na kuchukua fomu bila kujali wataambulia nini. Kila mmoja alikwenda kwa mbwembwe zake, lakini aliyetia fora na kupata coverage ya ajabu ni Augustine Mrema wa Tanzania Labour Party (TLP), ambaye aliwahi kuwania Urais mara mbili na kushindwa vbaya. Je mara hii mbwembwe zake zitamsaidia kuudaka Urais?.

2 comments:

Ndesanjo Macha said...

Reginald, asante kwa picha hiyo. Kweli siasa ni usanii pia.

Anonymous said...

Kwa mtindo huu, kama yangekuwa mapenzi yangu "Vyama vya Upinzani vyote mwaka huu ningevipeleka likizo ya miaka isiyopungua 10 ili vikakomae kisiasa, kutafakari kwa kina na kuwatupilia mbali wagombea wao wote wa urais na hasa wale ambao ni wenyeviti (Taifa) na walishawahi kugombea mara kadhaa na "kushindwa vibaya".

Mlinzikimenyi - Itabagumba/Buseresere

Thanks Miluko, your articles are ever awesome ... Keep it real

Post a Comment