Tuesday, October 11, 2011

Maakuli ya Kihaya

Hivi majuzi nikiwa kwenye likizo yangu ya mwaka nilifurahia sana maakuli haya yanayoandaliwa kwa taratibu na heshima zote za Kihaya baada ya kuyamisi kwa muda mrefu. Humo ndani kuna ndizi, nyama, maharage, nyana chungu, chumvi na maji. Chini yametangulizwa majani ya mgomba kuzuia kushika kwenye sufuria na juu kimefunikwa kwa majani hayo kuhifadhi mvuke ili chakula kiive taratibu. Watalaamu wa shughuli hii wanaonekana hapo nyuma wakisimamia kwa mbali...nadhani mnaelewa kuwa shughukli ni watu na watu wenyewe ndio hao. Picha zaidi fungua albam

No comments:

Post a Comment