Tuesday, October 04, 2011

Nakulilia mama yangu Tanganyika


Bendera yako hii Tanganyika ilikuwa na uzuri wa pekee, lakini wewe ukauawa na yenyewe ikapotezwa, ikazaliwa Tanzania. Hilo kwangu si tatizo, lakini kinachonisikitisha na kuniliza sana ni ile siku ya uhuru wako inayoadhimishwa kila mwaka, na hasa mwaka huu unapotimiza miaka 50 kubatizwa jina jipya , eti ni 'Siku ya Uhuru wa Tanzania Bara'...Wanaoimba wimbo huo wanajua fika kuwa wakati Mama yangu Tanganyika unapata uhuru Desemba 9, 1961 Tanzania ilikuwa haijazaliwa. Wanajua kuwa mwaka huu 2011 Tanzania (iwe bara au visiwani) haitakuwa imetimiza miaka 50. Ninakulilia sana Mama yangu Tanganyika. Hata kama umekufa, ukazikwa, waliofanya hicho kitendo watambue basi kwamba ulikuwapo na ulikuwa mama yetu kweli.

No comments:

Post a Comment