Kwa mujibu wa matokeo yaliyotolewa na mmoja wa makampeni meneja wake, Edward Kinabo,mpaka sasa katika kata 14, Mnyika anaongoza kwenye kata 12 kwa kumzidi mgombea wa CCM, Hawa Ng'umbi kura 16,732.

Matokeo ya kata 2 za Saranga na Kibamba bado yanaendelea kujumlishwa na timu yake inayotumia fomu za matokeo halali ya kila kituo yaliyotolewa na NEC.Wakati huo huo wagombea udiwani wa Chadema kata ya Ubungo, Sinza, Saranga, Goba, Mbezi, Makuburi na Kibamba wanatarajiwa kutangazwa washindi wakati wowote kuanzia sasa baada ya kuongoza kwa kura nyingi.

Matokeo rasmi ya ubunge yanatarajiwa kutangazwa leo baada ya Nec na vyama vyote kukamilisha ujumlishaji unaoanza alfajiri hii Mabibo katika ukumbi wa shule ya sekondari Loyola.

Source: Jamii Forum. Taarifa hii ni kwa mujibu wa Mnyika mwenyewe