Sunday, October 31, 2010

Breaking Newsssss

Uchaguzi majimbo matatu waahirishwa

Majimbo matatu ya Nkenge, Mpanda Mjini na Mpanda Vijijini hayakupiga kura za wabunge kwa kilichoelezwa na NEC kuwa ni kasoro zilizojitokeza, ukiwamo ukosefu wa karatasi za kura. Lakini karatasi za kura za udiwani na Urais zilifika bila matatizo.

Mbali na Majimbo hayo, zipo kata 23 ambazo hazikupiga kura za madiwani, ikiwamo Gongolamboto ya Dar es Salaam, Mirongo na Mkuyuni ya jijini Mwanza. Kuna taarifa kuwa majimbo mengine manne ya Zanzibar nayo yataongezeka. tarehe ya uchaguzi huo itatangazwa baadaye, na taarifa zaidi baadaye.

No comments:

Post a Comment