Monday, October 04, 2010

Mjadala wa Wanabidii

Nimekuta mjadala mtamu katika mtandao wa Wanabidii wakijadili mpango wa matokeo ya uchaguzi kupinduliwa. Ni mjadala mtamu kweli. Nimeushiriki, nikachangia hivi:

Tunashangaa nini matokeo kupinduliwa?

Mosi, Chama chenyewe ni cha MAPINDUZI, kwa hiyo kupindua matokeo si jambo la ajabu.

Pili, Viongozi wake wote wa juu ni Wanajeshi

Mwenyekiti: Luteni Kanali Jakaya Kikwete
Katibu Mkuu: Luteni Yusuf Makamba
Naibu Katibu Mkuu: Kapteni George Mkuchika
Katibu wa Itikadi/Uenezi: Kapteni John Chiligati
Meneja Kampeni: Kanali Abdulrahaman Kinana

Tatu, Gazeti la Serikali, Daily News ambalo Editor in Chief ni Rais, limeshasema: 'Dk. Slaa hatakuwa rais wa tano wa Tanzania'.

Nne: Tamko la Luteni Jenerali Shimbo linajieleza: "Wagombea wakubali matokeo, la sivyo..."

Tano: Katiba ya nchi/ sheria ya uchaguzi iko wazi: Matokeo ya urais yakishatangazwa, hakuna chombo chochote kinachoweza kuyapinga.

Nawasilisha

No comments:

Post a Comment