Thursday, September 23, 2010

Nilipotea Sana. Samahani

Wapenzi na wasomaji wa blog hii nawaomba radhi sana kwa kupotea bila kuaga kwa takriban wiki tatu. Niliondoka baada ya kupata msiba mzito wa baba yangu mzazi, Mzee Simon Kamuhabwa Miruko (pichani) ulitokea Septemba 2, 2010. Baada ya kutulia kiasi nilijaribu kuweka taarifa hapa kwa internet ya simu bila mafanikio. Lakini yote hayo ya Mungu, nimerejea tuendelee kupata mavituvitu.-RSM-

3 comments:

Anonymous said...

Bila samahani. Pole sana kwa msiba mzito uliokupata. Mwenyezi Mungu ampumzishe mzee mahali pema peponi na ampatie raha ya milele.
Kwa ninyi mliobakia, Mungu awapatie nguvu za kukabiliana na magumu ya kuondokewa na mzee. Awazidishie hekima na uwezo wake wa maarifa ili mfanikiwe zaidi katika maisha yenu yaliyobaki. Mkiwa na tumaini la kukutana na wale waliowatangulia siku moja.
Pole sana.

Anonymous said...

Pole kaka kwa msiba, Mungu akupe moyo wa subra.

"Nahakika kila nafsi itaonja mauti"

Anonymous said...

Pole sana. Mungu amlaze mahali pema katika ufalme wake.

Post a Comment