Wednesday, February 08, 2006

Rugambwa Atimiza Miaka Tisa Bila Kuzikwa


Ni miaka tisa sasa tangu Kardinali wa kwanza wa Afrika, Mwadhama Laurian Kardinali Rugambwa afariki dunia, mwaka 1997. mwili wake ulipumzishwa katika Kanisa la Kashozi km 15 Mashariki mwa Mji wa Bukoba, ukisubiri kuhamishiwa katika makazi yake ya milele katika Kanisa Kuu la Bukoba (katikati ya mji), alilochagua litumike kwa mazishi yake. Kanisa hilo bado linafanyiwa ukarabati mkubwa na wa muda mrefu, unaogharimu fedha nyingi ambazo waumini peke yao wameshindwa kukamilisha. Sina uhakika itachukua muda gani hadi Rugambwa kuzikwa rasmi, lakini wananchi, hasa waumini wa dini ya Kikatoliki wameanza kuhoji, kwa nini asizikwe muda wote huo? Kardinali Rugambwa ana Hitoria ndefu SOMA HAPA atakumbukwa kwa mengi, na baadhi ya watu wanasema alifaa kufanyiwa mchakato wa kutangazwa Mtakatifu, hata kabla ya mwalimu Julius Nyerere, Rais wa Kwanza wa Tanzania anayefanyiwa sasa.

3 comments:

Jeff Msangi said...

Miruko,
Hili nilikuwa silijui kwa hiyo lazima niseme ahsante sana kwa kuliweka hapa.Historia muhimu hii.

FOSEWERD Initiatives said...

masikini Rugambwa! mungu amlaze pema peponi. amen.

Anonymous said...

Miruko,
naomba ubadili kiungo cha masomo kwa wanablogu. Weka hiki:
http://mwongozo.wordpress.com

Ngoja nisome ile kuhusu Nyerere na utakatifu nami nichangie.

Post a Comment