Wednesday, August 25, 2010

Msafara wa JK waua mtoto

Habari zilizoifikia blogu hii jana jioni zinasema gari moja aina ya Land Cruiser VX, T 181 BJP, lililokuwa katika msafara wa Rais Jakaya Kikwete, jana liligonga na kuua mtoto wa shule, eneo la Izigo/Muhutwe, Muleba, mkoani Kagera. Hata hivyo, wahusika katika msafara huo wa mgombea urais kwa tiketi ya CCM walisema gari lililoua halikuwa katika msafara. Baadaye ilidhihirika kuwa gari hilo lilikuwa limeutangulia msafara wa JK; na lilibeba vifaa vya kampeni vya CCM. Dereva wa gari hilo alishikiliwa na kuhojiwa na polisi mkoani Kagera, lakini jitihada za kupata mamlaka husika kufafanua ajali hiyo hazikufanikiwa.

No comments:

Post a Comment