Thursday, July 29, 2010

Waziri Sitta mbaroni kwa rushwa

Waziri Mbaroni kwa rushwa

Na Chuma Shomari

WAZIRI wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto , Bi. Magreth Sitta jana alikamatwa na maofisa wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) baada ya kutuhumiwa kutaka kuwahonga wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Wanawake mkoani (UWT) Tabora ili wampatie kura.

Bi. Sitta alikamatwa katika nyumba ya kulala wageni ya Camise, iliyopo katika Mtaa wa Cheyo mjini hapa, ambapo alidaiwa kukutwa na pesa taslimu sh. milioni moja, simu saba za mkononi aina ya Nokia na akiwa na mipango ya kuzungumza na wajumbe wa mkutano huo kutoka katika wilaya ya Uyui mkoani Tabora. Isome zaidi.
Baadaye Mama Sitta alijibu mapigo kuwa hizo ni njama za kummaliza kisiasa, yeye na mumewe. Hii iko hapa.

No comments:

Post a Comment