Tuesday, June 15, 2010

Mkutano wa Bunge 'Umeisha'

Hivi sasa Bunge linajadili Muswada wa Sheria ya Fedha ya mwaka 2010 (Finance Bill Act 2010) iliyowasilishwa na Waziri wa fedha,. Sheria hii ndiyo hufanya marekebisho ya sheria mbalimbali ili kuruhusu mapendenezo ya yaliyopitishwa katika Bajeti ya Serikali hapo jana. Kwa maana hiyo, sheria hiyo ikipita baadaye leo, ikasainiwa na Rais, bajeti inaweza kuanza kutumika kuanzia Julai Mosi, 2010. Kwa maana hiyo mijadala ya bajeti za wizara ambazo hazijapita bunge, zinakosa maana...Hivyo, bunge ni kama limeisha.

No comments:

Post a Comment