Tuesday, June 01, 2010

Mchakato wa 'Kumtakatifuza' Nyerere


Rais Jakaya Kikwete na mwenyeji wake Rais Yoweri Museveni wa Uganda wakiagana na Mama Maria Nyerere muda mfupi baada ya kumalizika kwa misa Maalumu ya Kumwombea Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Nyerere ili atangazwe kuwa Mwenyeheri iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mashahidi wa Uganda huko Namugongo, nje kidogo ya mji wa Kampala jana. Misa hiyo iliyohudhuriwa pia na baadhi ya waumini kutoka Tanzania ni sehemu ya mchakato ulioanzishwa na Kanisa Katoliki Tanzania wenye nia ya kumtangaza Mwalimu Nyerere kuwa Mwenyeheri na hatimaye Mtakatifu kulingana na vigezo na kanuni zilizowekwa na kanisa hilo. (Picha na Freddy Maro)Rais Yoweri Museveni wa Uganda akisisitiza jambo wakati akizungumza na Rais Jakaya Kikwete muda mfupi baada ya ibada maalumu kumuombea Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliyofanyika katika Kanisa la Mashahidi wafia dini wa Uganda huko eneo la Namugongo, nje kidogo ya jiji la Kampala leo asubuhi.Wa kwanza kushoto ni Askofu Msaidizi Methodius Kilaini wa Jimbo Katoliki la Bukoba na wapili kushoto ni Dr.Cyprian Lwanga Askofu Mkuu wa Jimbo kuu Kanisa Katoliki Kampala.

No comments:

Post a Comment