Monday, November 02, 2009

Mbunge Sigfrid Ng'itu Afariki Dunia

Mbunge SIGIFRID SELEMAN NG'ITU,wa RUANGWA-CCM,LINDI, amefariki dunia. Kikao cha Bunge kimeahirishwa hadi kesho kutokana na msiba huo.

Mbunge huyo alikuwa amelazwa katika Taasisi ya Mifupa muhimbili (MOI) kutokana ugonjwa wa kiharusi, uliosababisha damu kuvilia kichwani, hivyo kufanyiwa upasuaji kutokana na tatizo hilo.

Spika wa Bunge, Samuel Sitta alisema jana kabla hajaahirisha bunge kuwa mbunge huyo pia alikuwa anasumbuliwa na tatizo la sukari na alipata malaria. Kamati ya bunge ya Utawala imekutana asubuhi hii kupanga taratibu za mazishi.

1 comment:

John Mwaipopo said...

bwana ametoa na bwana ametwaa jina lake lihimidiwe. sauti ya baragumu inawatakia wananchi wa jimbo la marehemu mbunge subira na nguvu, na juu ya yote uchapakazi mwema.

Post a Comment