Tuesday, October 27, 2009

Lowassa Kukabwa Koo

Urafiki wa Lowassa, JK usiingilie urais-Wabunge

*Selelii, Kimaro wataka afikishwe kortini
*Walaumu serikali kwa kutoa majibu ya ovyo
*Lowassa: Sizungumzi na vyombo vya habariWAKATI mkutano wa bunge unaanza leo, mzimu wa mkataba tata wa Richmond umeendelea kumwandama aliyekuwa Waziri Mkuu, Bw. Edward Lowassa baada ya baadhi ya wabunge kudai kuwa anastahili kuchukuliwa hatua zaidi ya ile ya kujiuzulu kutokana na kutajwa kwake katika kashfa hiyo.

Wabunge hao kwa nyakati tofauti wamesema kuwa urafiki ambao Bw. Lowassa alisema upo baina yake na Rais Jakaya Kikiwete usiingilie urais, serikali na uiachwe ifanye kazi yake kwa kumchukulia hatua kutokana na kuliingizia taifa hasara.
Endelea nayo

No comments:

Post a Comment