Mwanamuziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Mbilia Bel akiwapagawisha mashabiki waliohudhuria onyesho lake lililofanyika Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay jijini Dare es Salaam mwishoni mwa wiki. Hisani ya Celtel
Mbilia Bel, akiungana na wacheza shoo wake kushambulia jukwaa wakati wa shoo iliyofanyika Ijumaa usiku katika Bwalo la Maofisa wa Police Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Mashabiki wa musiki wakiwa wamevamia steji wakati wa Mwanamuziki nguli kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mbilia Bel akitumbuiza mwishoni mwa wiki katika Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Mbilia Bel na mwimbaji wake ambaye pia ni mcheza shoo, Theo Phille wakisakata rhumba wakati wa shoo ya mwanamama huyo
Mbilia Bel akimpagawisha mmoja wa mashabiki waliohudhuria onyesho lake lililofanyika Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oyster bay
Mwanadada Getrude Zongo akionyesha umahiri wa kucheza miondoko ya rhumba wa shoo ya mwanamuziki kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Mbilia Bel katika Bwalo la Maofisa wa Polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment