Friday, May 15, 2009

Mambo Yaiva Busanda

Habari zilizothibishwa ambazo zimetua mezani sasa hivi ni kuwa kilekikosi maalum cha CCM cha kupiga na kujeruhi mashabiki na wafuasi wavyama vya siasa vya upinzani kimewasili Busanda jana jioni.

Leo asubuhi takriban saa 5.40 (jana) vijana hao wa CCM wamewapiga vijanawaliowatuhumu kuwa wafuasi wa CHADEMA ambao walikuwa katika kiwanjaambacho mkutano wa kampeni wa CCM unafanyika.
Saa hizi mkutano huo unaendelea na viongozi kadhaa wa serikali wanatarajiwa kuhutubia mkutano huo.

Wakati huo huo jeshi la polisi limekamata pikipiki zote zinazotumiwana Chadema katika shughuli zake za kampeni katika kata za jimbo la Busanda kwa kisingizio cha kutokusajiliwa. CHADEMA walibuni mbinu ya kutumia pikipiki kwani sehemu kubwa ya jimbo la Busanda haifikiwi kwa magari. Souce: Bidii Forum

No comments:

Post a Comment