Thursday, May 14, 2009

Sala ya Chadema


Eee Mungu uliye Busanda, utusaidie sisi wa Chadema ili hawa watu wote wanaokuja kwenye mikutano yetu wawe wamejiandikisha kwenye daftari la wapiga kura. Mawazo yao yasibadilike hata akifika Anna Kilango na wabunge wenzake wanaojitangaza kuchukia ufisadi, ili ifikapo Mei 24 waweze kumchagua mgombea wetu na hiyo ndio iwe ishara yetu nzuri kuelekea Biharamulo Magharibi na hata Uchaguzi Mkuu 2010. Amen

1 comment:

Anonymous said...

chadema ni mafisadi na wataiharibu nchi,usalama wa taifa mko wapi,wawekeni ndani wote hawa,wameharibu tarime kisha wameingia mitini,wameacha wa kurya kule wanauwana wenyewe kwa wenyewe.sasa wanaingiza chuki na huku,ni aibu kwa viongozi wa chadema kukamatwa kwenye mkutano wa ccm wanazomea.cha ajabu wameenda mpaka kwa john cheyo kumuharibia,mtoa picha mbaya sana kwa nchi,hivi hamuoni kama cuf wanavyofanya kampeni za kistaarabu sana.sidhani chadema kama itakuwepo after 2010.maana hamuezi siasa,kazi kumwaga chuki,mtaiharibu nchi.

Post a Comment