Friday, April 24, 2009

Mzee Kabuye Is No More

Mzee Phares Kabuye, aliyekuwa mbunge wa Biharamulo Magharibi akiwa mbele ya nyumba yake mjini Biharamulo, Kagera tulipofanya mazungumzo naye wiki iliyopita. Leo amefariki katika ajali ya basi wakati anaelekea Dar es Salaam kwenye Mkutano Mkuu wa TLP. Katika Mkutano huo alisema angewania tena nafasi ya Makamu Mwenyekiti (Bara) na ujumbe wa Halmashauri Kuu (seneti). Nimeandika Obituary (tanzia) kwenye gazeti la Mwananchi. Isome hapa

5 comments:

Ngurumo said...

Reginald, Kabuye hakuwa Mbunge wa zamani wa Biharamulo Magharibi. La kujiuliza ni hili. Baada ya Kabuye ni nani alikuwa mbunge mpya wa Biharamulo Magharibi? Au tuseme nin nani alikuwa mbunge? Hakuna! Kabuye ndiye alikuwa the most recent MP wa jimbo hilo. Hivyo, si vema kumuita wa ZAMANI. Nadhani ni matumizi yenye kasoro ya neno hilo. Labda angetambulishwa kama ALIYEWAHI KUWA MBUNGE wa Biharamulo Magharibi! Unasemaje?

Baada ya hayo, RIP Mheshimiwa Kabuye!

Ngurumo said...

In fact, the most immediate former MP, Mr. Phares Kabuye... Hastahili kuitwa Mbunge wa ZAMANI. Wale wa zamani wapo. Si yeye; ingawaje sasa ana anuani mpya - hayati! Mungu amweke mahali pema! Alikuwa mwema; hakuwa fisadi.

Reginald said...

Point noted Ngurumo

John Mwaipopo said...

Reginald, kati ya vifo vya wabunge vilivyonihuzunisha cha Phares Kabuye ni kimojawapo. Pengine cha mwanzo.

Kifo ni kifo lakini hiki kimechagizwa. Sisemi kuna mkono wa mtu, sana sana kuna mkono wa mungu. Kesi yake ya ubunge ilianzishwa na wasiopenda maendeleo. ndio maana hata haikuvutia. Mzee kabuye alipendwa na wapenda maendeleo wote pasi na kujali itikadi za siasa zao. Alichukiwa na mafisadi. Hao ndio waliotaka kumtoa ubunge. Pengine wamefurahi sasa!

Kwa nini nasema alipendwa na wapenda maendeleo pasi itikadi. Bungeni haluonge ujinga kama baadhi ya wabunge wanavyoongea ujinga, tena na elimu zao ambazo marehemu hakuzifikia. Aliongea na kudadisi/kuuliza masuala ya kitaifa. Akiongea wote tuliona wasiopenda maendeleo wakimkalisha chini mara kwa mara eti kakosea hapa ama pale ilimradi wamchanganye na wapoteze mtiririko wa alichokuwa akikisimamia. pacha wake alikuwa marehemu chacha wangwe.kumbe naye hatunaye. jamani.

Wasiopenda maendeleo ndio walichagiza asimamishwe ubunge na ndio maana safari hii hakuwa dodoma kunakoendelea kikao cha bunge. wamefurahi sasa. Kinachonisikitisha hata nione kwa kifo chake is untimely ni kuwa pasi na kuwa na fitina za kisiasa na za kiubunge pengine mpiganaji huyu angetokea dodoma (si Biharamulo) ambako kuna bunge linaiendelea, kumbe angepanda basi ambalo dereva wake hajachola kwa safari ndefu, kumbe angeweza kufika salama dar es salaam, kumbe angekuwa hai kuendelea kulitetea taifa la wanyonge wengi, na wanyongaji wachache.

RIP Phares Kabuye

**********************************************

Miruko itundike humu obituary. Kwenye kiunganishi sijaipata.

Reggy's said...

Asante bwana mwaipopo. Naweka post yake hapo juu, maana mwananchi siku hiyo hawakuiweka hewani

Post a Comment