Saturday, February 28, 2009

Pinda akaiwa Dublin, Ireland

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na watangazaji wa Kituo cha Radio cha Digital Hub FM cha jijini Dublin baada ya kufanya mahojiano na Kituo hicho akiwa katika ziara nchini Ireland, Februari 27, 2009.(Picha zote na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Mizengo Pinda akizungumza na mmiliki wa Shamba la ng’ombe katika eneo la Ashtown, nje kidogo ya jiji la Dublin , Bw. Jimmy Tool (kulia kwake) baada ya kutembelea shamba hilo akiwa katika ziara ya kikazi nchini Ireland, Februari 27,2009. Kushoto ni Meneja wa Shamba hilo, Oliver Dollon

Mizengo Pinda akiwapa ng’ombe chakula baada ya kufurahishwa na ufugaji bora wakati alipotembelea shamba la Mzee, Jimmy Toll (kushoto) katika eneo la Ashtown nje kidogo ya jiji la Dublin nchini Irelanda akiwa katika ziara nchini humo Februari 27,2009. Ng’ombe hao wa maziwa hutoa zaidi ya lita 30 kwa siku.

Mizengo Pinda na ujumbe wake wakitembelea Kituo cha Mafunzo na Utafiti na Usindikaji Vyakula kilichopo Ashtown (Ashtown Food Research Centre) nje kidogo ya jiji la Dublin nchini IrelandNo comments:

Post a Comment